BOB CAT CHIPUKIZI WA HIP HOP ANAISAKA KOLABO YA JOH MAKINI KULIKO MSANII YEYOTE TZ


Chipukuzi mpya ndani ya bongo fleva katika miondoko ya Hip Hop HEAVENLIGHT MICHAEL A.KA. BOB CAT mwenye makazi yake Jijini Dar es salaam, ambaye hivi karubuni ameachia wimbo wake mpya alioupa jina la STRESS akiwa amemshirikisha LAVA LAVA ameiambia OBASCO ONE NEWS kuwa ndoto yake kubwa ni kufanya kazi ya pamoja na nguli wa Hip Hop nchini Joh Makini.

Akizitaja sababu za kuitaka kolabo ya Msanii huyo mkongwe Bob Cat ameuambia mtandao huu kuwa licha ya kuwa shabiki mkubwa wa muziki wake lakini kwa sasa Joh Makini ndio msanii pekee anayefanya vizuri kwenye tasnia hiyo jambo ambalo hulichukulia kama changamoto kubwa kwake

Licha ya kutokuwa na Meneja Bob Cat ambaye ana ndoto ya kuufikisha muziki wake kimataifa amewaomba watanzania hususani wapenzi wa muziki mzuri kumpokea kwa mikono miwili ili wapate kufaidi kazi nzuri kutoka kwake.

Chipukizi huyo ambaye anampango wa kuachia video ya nyimbo yake ya STRESS mwezi February mwaka huu, kwa sasa anapata pesa za kuendeshea muziki wake kupitia shughuli zake za Graphics na Upigaji Picha huku akiwa anaendelea na masomo ya chuo, amesema endapo ata tokea meneja atakuwa tayari kufanya nae kazi.

Unaweza kuusikiliza na kuu download nyimbo yake ya STRESS hapo chini

Usipitwe na chochote kutoka OBASCO ONE NEWS.

No comments

Disqus Shortname

LIVE COMMENTS

YOUR COMMENT OUR PRIORITY
kuuuuuuuuuuuuuuuuuuma. Powered by Blogger.